Mtu mmoja kwa jina Benard Shumba mkazi wa Singida anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa kumuua mke wake miaka nane iliyopita kisha kuuficha mwili kwenye mbuyu.

Mtu mmoja kwa jina Benard Shumba mkazi wa Singida anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa kumuua mke wake miaka nane iliyopita kisha kuuficha mwili kwenye mbuyu.
Ikiripotiwa na TBC Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida ,Deborah Magiligimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema mtuhumiwa baada ya kukamatwa alikiri kutenda kosa hilo na kwenda kuonesha mwili wa marehemu aliokuwa ameuhifadhi ndani ya mbuyu Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kupata mabaki ya mwili wa mwanamke huyo. Habari zaidi... Kuna tukio moja la MAUAJI lililotokea mwaka 2010 lakini mabaki ya mwili wa Marehemu yamepatikana leo jioni. Ni kwamba mnamo tarehe 7/10/2010 huko katika kijiji cha Yulansoni kata na tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida. Tabu Robert,mnyiramba,28yrs mkulima wa Yulansoni aliuawa na mume wake aitwae Bernard Shumba@Siza,mnyiramba,47yrs,mkulima wa Yulansoni. Baada ya Mtuhumiwa kufanya tukio hilo aliuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuuficha kwenye mti wa mbuyu ambao unatundu kubwa na kisha aliripoti polisi kituo kidogo cha Kinampanda Mkalama kuwa mke wake ametoroka na alianza kumtafuta hadi tarehe 17/3/2018 taarifa zilipopatikana kuwa alimuua. Baada ya Mtuhumiwa kukamatwa na kuhojiwa alikiri kufanya tukio hilo nakuonyesha sehemu alipomtupia.tarehe 18/3/3018 saa 16:00hrs OC CID Mkalama na timu yake ya makachero walifika eneo la tukio nakufanikiwa kupata mabaki ya mifupa yakiwa ndani ya mti huo. Baadhi ya mifupa imechukuliwa kwa ajili yakupeleka kwa mkemia wa serikali na iliyobakia ndugu wamekabidhiwa kwa ajili ya mazishi. Nini maoni yako juu yahili.

Comments

Popular posts from this blog

BASI LINGINE LA NEW FORCE LAPATA AJALI MBAYA.

DEATH OF JOHN RAMBO IS IT TRUE

DALILI 10 ZA KUACHA NA MPENZI WAKO