Hizi hapa sababu za mama yake Irene Uwoya Kuto hudhuria harusi yake na Dogo Janja.

Uwoya afunguka kwa
nini Mama yake kutoshiriki ndoa yake na Dogo Janja MUIGIZAJI wa Filamu Nchini Irene Uwoya amefunguka sababu za mama yake kutoshiriki kwenye ndoa aliyofunga hivi karibuni na mumewe Dogo Janja. Octoba 30 Mwaka jana wawili hao walifunga ndoa,ambayo ilihudhuriwa na watu wengi,lakini cha ajabu Mama Mzazi wa Irene Uwoya hakuwepo. Irene alisema kuwa Mama yake amekuwa ni mtu wa kusafiri mara kwa mara hiyo ndiyo sababu iliyopelekea Mama huyo kutoshiriki na kutomepeleka Dogo Janja nyumbani kwao. "Hakuwepo kwahiyo hakuweza kushiriki kwasababu mama angu ni mtu wa kusafiri sana kwahiyo hakuwepo Tanzania lakini ndoa ameibariki"Alisema Uwoya Aliongeza mara kwa mara mama yake amekuwa mtu wa kusafiri na mpaka sasa hajatulia kiasi ambacho anaweza kuamua kumpeleka Mumewe Dogo Janja,ingawaje Baba yake ndiye anayekuwepo Nyumbani. Hata alivyoulizwa kutokuwepo kwa ndugu zake kwenye ndoa yake Irene alieleza kuwa ndugu zake walikuwepo baadhi japo hawakuwa wengi.

Comments

Popular posts from this blog

BASI LINGINE LA NEW FORCE LAPATA AJALI MBAYA.

DEATH OF JOHN RAMBO IS IT TRUE

DALILI 10 ZA KUACHA NA MPENZI WAKO