Al Qaeda Ya Pamba Moto upya, Huyu apa kiongozi Mpya na Mikakati yake.

Mtoto wa Osama Ateuliwa kua kiongozi wa kundi la Al Qaeda Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda, Osamba Bin Laden ali wahi kutoa ujumbe wa vitisho kwa Marekani kuhusu mpango wa kundi hilo kulipiza kisasi juu ya kifo cha baba yake Ameteuliwa kua kiongozi wakundi hilo. Hamza bin Laden ameapa kuliendeleza kundi hilo na kwamba watatekeleza shambulizi lingine linalofanana na lile la Septemba 11, mwaka 2001 lililotumia ndege mbili kushambulia makao makuu ya ulinzi ya Marekani. Marekani ilimsaka na kufanikiwa kumuua Osama Bin Laden kwa kutumia kikosi maalum katika maficho yake Abbottobad nchini Pakistan, Mei 2 mwaka 2011. Hamza bin Laden anajinadi kuwa “sisi sote ni Osama.” Mwaka 2008, Mbunge wa zamani wa Uingereza, Patrick Mercer alimtaja Hamza kama mtoto wa falme za kigaidi (the crown prince of terror). Barua iliyokutwa katika jumba alilouawa Osama Bin Laden ilionesha kuwa alipanga kumrithisha Hamza utawala wa kundi hilo baada ya kifo cha kaka yake Saad mwaka 2009 katika shambulizi lililofanywa na ndege zisizo na rubani za Marekani. Mpendwa msomajiwangu Naomba u subscribe hapojuu kisha ingia kwenye Menyu upande wakushoto kisha bonyeza Following kuni Follow.

Comments

Popular posts from this blog

BASI LINGINE LA NEW FORCE LAPATA AJALI MBAYA.

DEATH OF JOHN RAMBO IS IT TRUE

DALILI 10 ZA KUACHA NA MPENZI WAKO