Jacob Zuma Apatikana na makosa 16 ya rushwa.

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepatikana na mashtaka 16 ya rushwa inayohusishwa na mamilioni ya dola yaliotumika katika mpango wa silaha. Ikiripotiwa na BBC Mashtaka hayo ambayo bwana Zuma amekataa kuhusika yanajumuisha udanganyifu aliofanya ili kujipatia fedha na utakatishaji wa fedha. Bwana Zuma mwenye umri wa miaka 75,chama chake cha ANC kilimlazimishaa kuachia madaraka yake mwezi uliopita. Zuma alipigiwa kura ya kutoamaniwa mara ya tisa katika bunge kabla hajaachia ngazi. Mwendesha mashtaka mkuu Shaun Abraham amesema anaamini kuwa kuna sababu ya kuwa na mtazamo chanya juu ya hukumu ya kesi hii Bwana Zuma anatuhumiwa kutaka rushwa kutoka kwa Thales kwa nia ya kuboresha maisha yake ya kifahari.Mshauri wake wa fedha wakati huo alikutwa na hatia ya kuomba rushwa hizo mwaka 2005 na bwana Zuma alimfukuza kazi yake ya usaidizi wa rais. Mashtaka ya awali dhidi ya bwana Zuma yalikuwa yameondolewa muda mfupi kabla ya kuwa rais mwaka 2009. Kwa sasa anakabiliana na shitaka moja la kusababisha ghasia,mashtaka mawili ya rushwa,shtaka moja la rushwa na mashtaka 12 ya udanganyifu. Asante kwa kusoma taarifahii. Naomba usabscribe hapo juu Na uende kwenye menyu hapo uni follow asante kwa support yako.

Comments

Popular posts from this blog

BASI LINGINE LA NEW FORCE LAPATA AJALI MBAYA.

DEATH OF JOHN RAMBO IS IT TRUE

DALILI 10 ZA KUACHA NA MPENZI WAKO